KITAIFA

CHE MALONE KUTIMKIA LIGI KUU YA ALGERIA

che malone

Beki wa kati wa klabu ya Simba raia wa Cameroon Che Malone Fondoh huwenda akaondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya USM Alger inayoshiriki ligi kuu Nchini Algeria.

Mchezaji huyo aliyejiunga na Simba Julai 2023 akitokea Cotton Sport ya ligi kuu Nchini kwao anaondoka Simba kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa zinasema wekundu hao wa msimbazi tayari wamepata mbadala wa beki huyo na wapo katika hatua nzuri ya kumalizana naye ili kurithi mikoba ya Che Malone aliyekuwa chaguo la kwanza la Kocha Fadlu.

Leave a Comment