NAHODHA wa Simba SC, Mohamed Hussen msimu wa 2024/25 kuna uwezekano mkubwa akaibukia ndani ya kikosi cha Yanga SC akiwa ni mchezaji huru.
Ikumbukwe kwamba Zimbwe aliongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba SC mwaka 2023 tayari 2025 umefikika tamati Julai 10 2025 hivyo kwa sasa mchezaji huyo ni huru.
Julai 19 2025, Zimbwe Jr aliandika ujumbe wa kuwashukuru Simba SC akiwaaga mashabiki na wachezaji aliokuwa nao ndani ya kikosi cha Simba SC.
Kuna asilimia kubwa Zimbwe Jr akatambulishwa ndani ya Yanga SC akiwa ni mchezaji huru kwa kuwa taarifa zinaeleza kuwa wamefikia hatua nzuri kwenye mazungumzo.
Rekodi zinaonyesha kuwa msimu wa 2024/25 ndani ya ligi, Zimbwe alicheza mechi 27 kati ya 30 akikosekana kwenye mechi tatu na alifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.
Hivi karibuni Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC aliweka wazi kuwa mkataba wa mchezaji huyo umeisha na hajaongeza mkataba. Kitakachotokea itakuwa ni maslahi ya pande zote mbili.