FADLU Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC amekabidhiwa rungu la kufanya maamuzi kwa wachezaji ambao wanapaswa kuondoka katika kikosi hicho na wale ambao watabaki kwa msimu wa 2025/26.
Miongoni mwa wachezaji ambao Fadlu amebainisha kwamba anahitaji wabaki inaelezwa ni beki Mohamed Hussen ambaye mkataba wake umeisha akiwa anatajwa kuwa katika rada za Yanga SC.
Kocha huyo alifanya kikao na Rais wa Simba SC, Mo Dewji hivyo kuna uwezekano mkubwa akaendelea kuwa katika kikosi hcho kwa msimu mpya wa 2025/26.
Muda mfupi walipokutana Mo aliandika namna hii: “Tulia. Tathmini. Panga upya. Nimefurahi kuwa na mazungumzo ya maana na Kocha Fadlu katika msimu wake wa kwanza, akiwa na kikosi kipya na benchi jipya la ufundi, ameiongoza Simba SC kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.
“Chini ya Kocha Fadlu Davids, Simba imefika fainali ya CAF Confederation Cup, fainali ya pili ya kimataifa katika historia ya klabu. Msimu huu ulikuwa wa kujenga timu. Na bado tukafika fainali, licha ya upinzani mkali. Simba haitazuilika msimu ujao.”
Nataman kuona timu zinafanya usajili mzuri wenye hadhi ya FIFA ili tuongeze alama kwenye rank za CAF Kupitia timu zitakazoshirik mashindano ya kimataifa msimu ujao