Nani kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa FIFA leo

Washindi wa Tuzo za Mchezaji Bora za FIFA za mwaka 2025 watatangazwa usiku wa leo Jumanne, Desemba 16, mjini Doha, Qatar.

Washindi katika vipengele mbalimbali akiwemo Mchezaji Bora wa Kiume na Wanawake wanatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Walioteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa FIFA wa Wanaume ni pamoja na Ousmane Dembélé, Achraf Hakimi, Harry Kane, na Kylian Mbappé.

Walioteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa FIFA wa Wanawake ni pamoja na Sandy Baltimore, Nathalie Bjorn, Aitana Bonmatí, na Lucy Bronze.