MABINGWA mara 31 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC inatajwa kuwa imefikia makubaliano na kiungo mshambuliaji wa Tabora United, Offen Chikola kwa ajili ya msimu ujao baada ya kufikia makubalian mazuri.
Tetesiz za hivi karibuni zilieleza kiungo huyo kuwepo katika mazungumzo na Simba kwa ajili ya kuiimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo, katika msimu ujao wa 2025/26.
Kiungo tayari amemalizana na Yanga SC kwa kumpa mkataba wa miaka miwili, ambao utaanza kufanyakazi katika msimu ujao hivyo kuna uwezekano akapishana na Simba SC ambao walikuwa wanampigia hesabu.