Rulani Mokwena ametambulishwa rasmi na MC Alger kuwa kocha mkuu wa Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Nchini Algeria akichukua nafasi ya Khaled Ben Yahiam aliyepewa mkono wa kwaheri hivi karibuni.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 38 raia wa Afrika Kusini ambaye ambaye alikuwa anakinoa kikosi cha Wydad Casablanca msimu uliopita amepewa mkataba wa miaka miwili ndani ya klabu hiyo MC Alger atakaoanza kuutumikia kuanzia msimu ujao.