Klabu ya Simba Queens imetangaza kuachana na wachezaji 11 waliohudumu katika kikosi chao katika misimu iliyopita.
Wachezaji hao ambao wamepewa mkono wa kwaheri na wekundu wa msimbazi ni Precious Christopher, Asha Djafar, Riticia Nabossa, Saiki Atinuke, Josephine Julius, Gelwa Yona, Asha Mwalala, Jackline Wilbert, Daniela Ngowi, Wincate Kaari na golikipa Caroline Rufaa.