KITAIFA

KINACHOENDELEA KAMBINI KWA TAIFA STARS, MISRI

Taifa Stars

KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinaendelea na mazoezi kwenye kambi yake nchini Misri kujiandaa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zinazotarajiwa kuanza Agosti 2 hadi 30, mwaka huu.
Taifa Stars imekuwa ikifanya mazoezi viwanja vya Mercure Jijini Ismailia, Misri tangu iwasili Julai 8 kujiandaa na fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda.

Kikosi kipo chini ya Kocha Mkuu, Hemed Suleiman Ali ‘Morocco’ anayesaidiwa na wazawa wenzake, Juma Ramadhani Mgunda ‘Pep Guardiola Mnene’ na Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’ na kinaundwa na wachezaji 27 kutoka klabu tofauti nchini.

Hao ni pamoja na makipa Aishi Salum Manula ‘Air Manula’ wa Simba SC atakayekuwa pamoja na Hussein Masalanga wa Singida Black Stars na Yakoub Suleiman Ali wa JKT Tanzania.

Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba SC), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Mohamed Hussein (Simba SC), Pascal Msindo (Azam FC), Ibrahim Hamad ‘Bacca’ (Yanga SC), Dickson Job (Yanga SC), Wilson Nangu (JKT Tanzania). Abdurazak Mohamed (Simba SC), Vedastus Masinde (TMA Stars) na Lameck Lawi (Coastal Union).

Viungo wa katikati ni Ahmed Pipino (KMC), Mudathir Yahya (Yanga SC) na Yusuph Kagoma (Simba SC) — wakati viungo washambuliaji ni Nassor Saadun (Azam FC), Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC) na Feisal Salum (Azam FC).
Wengine ni Kibu Dennis (Simba SC), Jammy Simba (KMC), Sabri Kondo (Coastal Union), Shekhan Khamis (Yanga SC) na Abdul Suleiman ‘Sopu’ (Azam FC), wakati washambuliaji ni Clement Mzize (Yanga SC), Mishamo Michael (Ken Gold) na Ibrahim Hamad Hilika (Tabora United).

Taifa Stars imepangwa Kundi B pamoja na Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), wakati Kundi A kuna Kenya, Morocco, Angola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia.
Kundi C linazikutanisha Uganda, Niger, Guinea, Algeria na Afrika Kusini wakati Kundi D kuna Senegal, Kongo, Sudan na Nigeria.

Leave a Comment