KITAIFA

ZAMBIA NA MOROCCO WAIANZISHA WAFCON KWA SARE

Wafcon

Mchezo wa Ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake (WAFCON) kati ya timu ya Taifa ya Zambia dhidi ya wenyeji Morocco umemalizika kwa sare ya 2-2.

Kwenye mchezo huo. Magoli ya timu ya Taifa ya Zambia yalifungwa na nahodha Barbra Banda na Rachel Kundananji huku ya Morocco yakifungwa na nyota wao Ibtssam Jraidi na Chebbak.

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Twiga Stars’ watacheza mchezo wao wa kwanza wa makundi siku ya kesho Jumatatu ya Julai 7 dhidi ya timu ya Taifa ya Mali.

Leave a Comment