Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania @taifastars_ Nassor Saadun ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Azam FC hadi mwaka 2027.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ameongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi kuwatumikia matajiri wa Chamazi kwani mkataba aliokuwa nao awali ulikuwa unatamatika Juni 2026 kabla ya kuongeza mwingine.