KITAIFA

SIMBA BADO HAIJABADILIKA HATAKAMA IMESHINDA DHIDI YA AZAM

LICHA yakupata ushindi mechi tatu na sare moja bado Simba matatizo yake ni yaleyale lazima yafanyiwe kazi katika ulinzi na umaliziaji nafasi ambazo wanazitengeneza.

Mechi mbili Simba imepata ushindi katika matukio ambayo yamekuwa na utata kama ilivyokuwa dhidi ya Tabora United kisha dhidi ya Azam FC bao ambalo lilikataliwa lingebadili mchezo Mzizima Dabi.

Mchezo dhidi ya Namungo mawasiliano yalikuwa hafifu hivyo wakajifunga. Timu imeshinda mashabiki wanamtaja Juma Mgunda ambapo maombi yao ni kuona kwamba anakabidhiwa timu jumlajumla.

Bado Simba ni ileile ambayo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo hivyo ni muhimu kufanyia kazi makosa yake kwa umakini kuendelea kuwa bora kwa kuwa kushinda kwenye mechi kubwa haina maana kwamba matatizo yamekwisha.

Ikumbukwe kwamba ushindi sio sababu yakuficha makosa yaliyopita bali ni muhimu kufanyiwa kazi kwa umakini ili kuwa bora zaidi kwenye mechi zinazofuata pamoja na mashindano mengine.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba kuhusu mwendo wa timu hiyo amebainisha kwamba kwa sasa unazidi kuimarika mapungufu yatafanyiwa kazi.

“Tulikuwa kwenye mwendo mbaya na tulivurugwa vibayavibaya, kwa sasa taratibu tunazidi kuimarika kwa kuwa uwepo wa Juma Mgunda umetuliza yale mawimbi yaliyokuwa baharini na wachezaji wanacheza.

“Mashabiki tuzidi kuwa pamoja kwa kuwa bado hatujamaliza na malengo yetu ni kuona kwamba tunarejesha furaha na kuwa pamoja kwenye nyakati zote.”

Katika mechi nne ambazo ni dakika 360 Simba kwenye msako wa pointi 12 imesepa na pointi 10 ikipishana na pointi mbili.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button