JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA
Simba itakuwa uwanjani leo Jumatano kwa mara ya kwanza tangu itoke kambini Misri, lakini baada ya mshambuliaji Jonathan Sowah, kuna staa mwingine inaweza kumkosa mbele ya Yanga. Simba itamkosa Sowah kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, lakini mashabiki wa timu hiyo watamuona mshambuliaji huyo raia wa Ghana kwenye mchezo wa leo wa Tamasha la Simba Day:
Baada ya Simba Day leo, Septemba 16, 2025 Simba itakutana na Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii. Wakati leo Simba ikiadhimisha Tamasha la Simba Day pale Uwanja wa Benjamin Mkapa, taarifa mbaya ni kukosekana kwa kiungo fundi wao mpya Mohammed Bajaber.
Taarifa kutoka Simba ni, Bajaber aliumia tangu akiwa nchini Misri kwenye kambi ya wekundu hao iliyohitimishwa Agosti 28 mwaka huu. Staa huyo aliyesajiliwa na Simba kutoka Kenya Police FC, ataukosa pia mchezo wa leo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Gor Mahia kutoka Kenya kutokana na majeraha hayo. Kiungo huyo ambaye licha ya leo kutambulishwa lakini anatarajiwa kutocheza mechi hiyo ya kirafiki.
Source: Sports Arena