KITAIFA

MBEBA MIKOBA YA CHAMA KWENYE MTEGO SIMBA SC

simba

KIUNGO wa Simba SC, Deborah Mavambo ambaye ni ingizo jipya katika kikosi hicho kwa msimu uliogota mwisho wa 2024/25 yupo kwenye mtego ndani ya kikosi hicho kutokana na kiwango chake kuporomoka mwanzo mwisho.

Nyota huyo kwenye mechi za awali alianza kuonyesha ubora wake lakini kadri siku zilivyokuwa zinazidi uwezo wake ulikuwa unaporomoka. Atakumbukwa kwenye mchezo wa Simba Day, jina lake liliimbwa kutokana na kiwango bora katika matumizi ya nguvu kwenye mguu wake wa kulia.

Ni jezi namba 17 alikabidhiwa ambayo ilikuwa inavaliwa na kiungo Clatous Chama ambaye yupo ndani ya Yanga SC kwa msimu wa 2024/25. Mavambo alikuwa anapewa nafasi kufanya vizuri kitaifa na kimataifa mwisho akajenga ushikaji na benchi.

Mchezo wa mwisho wa Kariakoo Dabi, dhidi ya Yanga SC Juni 25 2025 hakupata nafasi yakucheza mchezo huo jambo ambalo linaonyesha kuwa ni mtego kwake.

Taarifa zinaeleza kuwa kuna wachezaji ambao watakutana na Thank You ndani ya kikosi cha Simba SC kutokana na kushindwa kuwa katika ubora huku jina la Mavambo likitajwa.

Leave a Comment