Droo ya makundi ya Kombe la Dunia 2026 imepangwa kufanyika tarehe 5 Disemba 2025 katika Kituo cha Kennedy, Washington DC Nchini Marekani.
Mashindano hayo yanayofanyika mara ya 23 yataandaliwa kwa mara ya kwanza na mataifa matatu ambayo ni Marekani,Mexico na Canada ๐จ๐ฆ, yakihusisha timu 48 kwa mara ya kwanza katika historia.
Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi rasmi Juni 11 hadi julai 19 mwaka 2026.
