Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home ยป GIFT FRED: BEKI WA YANGA APATA DILI NONO
    TETESI ZA SOKA

    GIFT FRED: BEKI WA YANGA APATA DILI NONO

    ChikaoBy ChikaoJune 9, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    BEKI wa zamani wa Yanga SC Gift Fred ambaye alishindwa kupata namba kikosi cha kwanza na kupewa Thank You anatajwa kupata dili nono kwa ajili ya changamoto mpya.

    Gift Fred anakaribia kujiunga na Klabu ya KCCA ya nchini Uganda katika msimu ujao wa 2025/26 kwa ajili ya kutimiza majukumu yake.

    Gift anakwenda kujiunga na KCCA akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mkopo St George ya nchini Ethiopia kumalizika.

    Ni Yanga SC ya Tanzania ilimpeleka beki huyo kwa mkopo St Georgeย  baada ya kutovutiwa na kiwango chake akishindwa kuwapa ushindani Ibrahim Bacca, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.

    Gift alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 2023 alikwama kuonyesha uwezo katika mechi za ushindani.

    Kwa sasa kwenye eneo la beki wa kati chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Yanga SC ni Dickson Job ambaye huyu anatajwa kuwa ataongezewa kandarasi nyingine kubaki ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleKAIZER CHEIF WAWEKA MZIGO KUMPATA AHOUA
    Next Article BAADA YA KUONA FEI TOTO ANAWEZA KUSEPAโ€ฆAZAM WAHAMISHA NGUVU KWA STAA WA SIMBA

    Related Posts

    TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI TAREHE 25.4.2025

    April 25, 2026

    SIMBA MBONI KUMALIZANA NA BEKI HUYU WA KAZI KUTOKA AL HILAL

    January 11, 2026

    Rasmi Clatous Chama Atibitisha Kurejea Simba

    January 2, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    IBENGE AKIRI KUTORIDHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

    matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026

    YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO

    SIMBA YASHIKA NAFASI YA 19 DUNIANI, IPO LEVO ZA MADRID

    HILI HAPA DAU LA KUMPATA COLE PALMER

    TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI TAREHE 25.4.2025

    PRESHA YA KUUKOSA UBINGWA YATAWALA REAL MADRID

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.