Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO
    Habari za Michezo

    YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO

    ChikaoBy ChikaoApril 25, 202604 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KUNA mchezo mmoja wenye hadhi ya fainali utakaopigwa leo Uwanja wa Amaan kuanzia saa 2:15 usiku na Azam FC itakutana na bingwa mtetezi wa Kombe la Muungano, Yanga, katika nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo.

    Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kufuzu hatua hii baada ya kuifunga Muembe Makumbi City mabao 4-0 katika robo fainali, huku Azam ikifuata siku moja baadaye kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ.

    Yanga inalenga kutetea taji hilo ililochukua msimu uliopita ilipoifunga JKU bao 1-0, wakati Azam ikisaka kuandika historia kwa kushinda ubingwa wake wa kwanza wa Kombe la Muungano.

    Msimu huu, timu hizi zimekutana mara mbili. Mara ya kwanza ilikuwa kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi na Yanga ilishinda kwa penalti 5-4 baada ya sare ya dakika 120, na mara ya pili walikutana kwenye ligi na mchezo ulimalizika kwa sare tasa.

    Katika ligi kuu, zote bado hazijapoteza mchezo wowote hadi sasa, jambo linaloonyesha uimara wao. Matokeo yao mabaya yamekuwa ni sare pekee, hali inayoongeza ushindani kuelekea pambano hili.

    Rekodi zinaonyesha nje ya ligi wamekutana mara 17 katika mashindano mbalimbali; Yanga ikishinda mechi 10, Azam ikishinda tano huku sare zikiwa mbili.

    Yanga inatambua kwamba itakuwa na mchezo mgumu dhidi ya Simba, Mei 3 mwaka huu, lakini bado imekuwa haitaki utani ikiwatumia mastaa wake muhimu kama ambavyo ilifanya dhidi ya Muembe Makumbi City.

    Yanga imeonyesha kutokuwa na mzaha kwa kuendelea kutumia kikosi chake bora licha ya ratiba ngumu, ikiwa pia inajiandaa na mchezo mkubwa wa ligi dhidi ya Simba Mei 3.

    Kwa upande wa Azam, timu hiyo imeonyesha nia ya kweli ya kulichukua kombe hili baada ya kuwapumzisha baadhi ya mastaa wake muhimu katika mechi iliyopita.

    Wachezaji kama Feisal Salum ‘Fei Toto’, Idd Seleman ‘Nado’, kipa Aishi Manula pamoja na mabeki Lusajo Mwaikenda na Fuentes Mendoza wanatarajiwa kurejea kikosini leo.

    Washambuliaji Prince Dube na Jean Ngita ndio vinara wa mabao kwenye mashindano haya, kila mmoja akiwa na mabao mawili.

    Vita nyingine itakuwa eneo la kiungo ambapo endapo Fei Toto atakuwa uwanjani anayeongoza kwa asisti kule ligi kuu akiwa nazo saba, basi kuna uwezekano watakumbushia tena mbio zao za kutengeneza asisti kati yake na Allan Okello wa Yanga ambaye kwenye mashindano haya tayari anayo moja. Kwenye ligi anazo sita, moja nyuma ya Fei Toto.

    Kwa Yanga, Duke Abuya, Mudathir Yahya, Mohamed Damaro na Maxi Nzengeli wanatarajiwa kuongoza eneo la kati.

    Azam chini ya Ibenge, tunaweza kuona sapraizi huenda atampa nafasi Adolf Mtasingwa ambaye sasa yupo fiti baada ya kupona majeraha na tayari amecheza dhidi ya KVZ, pia mkata umeme mwingine, Sadio Kanoute yupo tayari kwa mapambano.

    Kwa ubora wa majina haya, eneo la kiungo linaonekana kuwa uwanja wa mapambano makali kati ya wakabaji na watengenezaji wa mashambulizi, hali itakayoweza kuamua matokeo ya mechi.

    WASIKIE WENYEWE

    Kocha wa Azam, Florent Ibenge alisema:

    “Kesho (leo) ni mchezo mkubwa kila mmoja anajua kwa sasa kwenye ligi yetu kule Yanga ndio timu bora kwa takwimu, sisi Azam tunafahamu tunakwenda kukutana na timu ngumu yenye hadhi hiyo kwenye mchezo wa nusu fainali,” amesemaIbenge.

    “Sisi (Azam) tunapenda kucheza mechi ngumu kama hizi, nawapongeza sana wachezaji wangu kwa kujituma na kufikia hatua hii, tumejiandaa kucheza kama ambavyo tumekuwa tukicheza, tutawapa nafasi wachezaji ambao tunaamini wataweza kutupa matokeo mazuri, najivunia wachezaji wangu haijalishi ni vijana au wale wakongwe.”

    Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves alisema:

    “Kesho (leo) ni nusu fainali tutakutana na Azam FC, moja ya timu bora zinazowania mataji hapa Tanzania, ni timu yenye nguvu, iliyofanya uwekezaji mkubwa, wanaohtaji mashindano kama haya kuthibitisha ubora wao, yenye wachezaji wazuri na kocha mwenye wasifu mkubwa kwenye soka la Afrika,” amesemaGoncalves.

    “Tunatarajia mchezo mgumu, tunatakiwa kuwa tayari kukabiliana nao, tunapita kwenye ratiba ngumu ya mashindano, sasa tuna mchezo wa nusu fainali na baada ya hapo tukishinda tutakwenda kwenye fainali tukimaliza mashindano haya tutakuwa na mchezo mgumu wa ligi dhidi ya Simba, lakini ni motisha kwetu kucheza dhidi ya wapinzani wetu wakubwa, tukiwa na akili ya kushinda hizo mechi.”

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleSIMBA YASHIKA NAFASI YA 19 DUNIANI, IPO LEVO ZA MADRID

    Related Posts

    SIMBA YASHIKA NAFASI YA 19 DUNIANI, IPO LEVO ZA MADRID

    April 25, 2026

    TAREHE PAMOJA NA UWANJA AMBAO DABI YA KARIAKOO ITAPIGWA

    April 24, 2026

    SIMBA SC YAWINDA MAJIBU KWA MLANDAGE, SI KISASI

    April 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO

    SIMBA YASHIKA NAFASI YA 19 DUNIANI, IPO LEVO ZA MADRID

    HILI HAPA DAU LA KUMPATA COLE PALMER

    TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI TAREHE 25.4.2025

    PRESHA YA KUUKOSA UBINGWA YATAWALA REAL MADRID

    TAREHE PAMOJA NA UWANJA AMBAO DABI YA KARIAKOO ITAPIGWA

    SIMBA SC YAWINDA MAJIBU KWA MLANDAGE, SI KISASI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.