Chelsea FC wanaweza kufikiria kumuachia Cole Palmer endapo ofa kubwa ya takribani £130M (karibu Tsh bilioni 410+) itawasilishwa majira haya ya joto.Kwa sasa, Real Madrid na Paris Saint-Germain ndizo klabu zinazotajwa kuwa na uwezo wa kufikia thamani hiyo.
Palmer, aliyesajiliwa kwa £42.5M, angeleta faida kubwa sana kwa Chelsea, lakini uamuzi huo unaweza kuathiri moja kwa moja ubora wa kikosi kwani ni miongoni mwa wachezaji muhimu zaidi.Kukosekana kwa nafasi ya UEFA Champions League kunaweza kuilazimisha Chelsea kufanya maamuzi magumu ya kifedha na kiufundi ili kujenga upya kikosi
