Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » BAADA YA KUONA FEI TOTO ANAWEZA KUSEPA…AZAM WAHAMISHA NGUVU KWA STAA WA SIMBA
    KITAIFA

    BAADA YA KUONA FEI TOTO ANAWEZA KUSEPA…AZAM WAHAMISHA NGUVU KWA STAA WA SIMBA

    ChikaoBy ChikaoJune 9, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    HAWAJAWEKA wazi lakini tafsiri ya kiufundi ni kwamba Azam FC wako kwenye harakati za kujiandaa na lolote kwenye nafasi ya Feisal Salum ‘Fei Toto’

    Staa huyo ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Azam amekuwa akihusishwa na kujiunga na Simba, Yanga na Kaizer Chiefs msimu ujao ambapo kila mmoja kwa wakati wake anapambana kupata ahueni ya dau. Azam wamekuwa wakisisitiza kwamba mchezaji wao anauzwa kwa zaidi ya Sh1 bilioni.

    Ili kuziba pengo lake, Azam FC iko kwenye mazungumzo na Vipers ya Uganda kuhusu kiungo wake Allan Okelo  ambaye Simba pia iliwahi kumtaka, lakini ilijibiwa kwamba mchezaji huyo hauzwi.

    Hapo awali  kikosi hicho kilipiga hesabu kubwa za kumsajili kiungo mshambuliaji, Okello ambaye naye ni fundi wa mguu wa kushoto kama ilivyo Elie Mpanzu.

    SIMBA ILIFELI HAPA

    Wekundu hao wa Msimbazi walimtaka Okello, kama kiungo mshambuliaji kupitia dirisha dogo la usajili lililofunguliwa Desemba 15 mwaka jana.

    Utata kwa Simba kumpata Okello,ukawa kwa Rais wa klabu hiyo Lawrence Mulindwa, ambaye amekuwa mgumu kuachia mastaa wake muhimu wa kikosi hicho kuuzwa.

    Taarifa za ndani kutoka Uganda zilisema kuwa: “Tumeanza mazungumzo na Azam wakimhitaji Okello, hatujamalizana lakini ni mazungumzo pekee ambayo hatujafikia mwisho.

    “Unajua Okello anatakiwa na klabu nyingi, lakini hata sisi Vipers tunahesabu naye tutaona kipi tutafikia makubaliano kati yetu na Azam.”

    Vipers inashika nafasi ya kwanza katika ligi ya Uganda ikiwa imecheza mechi 30, ikishinda 21,sare sita na kupoteza mitatu,huku Azam ikiwa namba tatu katika msimamo ikisalia na mechi mbili mkononi kati ya 30, huku Okello akiwa amefunga mabao 19 ndani ya msimu mmoja ambao huu ni wa pili tangu alipoanza kuitumikia Vipers katika mashindano hayo.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleGIFT FRED: BEKI WA YANGA APATA DILI NONO
    Next Article YANGA YAIJIBU TFF, DAWA YA DENI NI KULIPA KWA WAKATI

    Related Posts

    IBENGE AKIRI KUTORIDHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

    April 26, 2026

    matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026

    April 26, 2026

    YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO

    April 25, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    IBENGE AKIRI KUTORIDHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

    matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026

    YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO

    SIMBA YASHIKA NAFASI YA 19 DUNIANI, IPO LEVO ZA MADRID

    HILI HAPA DAU LA KUMPATA COLE PALMER

    TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI TAREHE 25.4.2025

    PRESHA YA KUUKOSA UBINGWA YATAWALA REAL MADRID

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.