Rasmi michuano mikubwa ya soka barani Arika, Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2025) itaanza kutimua vumbi nchini Morocco kuanzia usiku wa leo Jumapili.
Morocco ambao ni wenyeji wa mashindano watashuka uwanjani Prince Moulay Abdellah huko Rabat kurusha kete yao ya kwanza wakati itakapokipiga na Comoros.
Morocco inashika nafasi ya 11 kwenye viwango vya soka vya dunia, huku ikishika namba moja kwa Afrika, wakati Comoros yenyewe inashika nafasi ya 108.
Timu hizo mbili zimewahi kukutana mara nne, ambapo Morocco ilishinda tatu na moja ilimalizika kwa sare.










Leave a Reply