Home KIMATAIFA MOURINHO ATAJWA KUCHUKUA MIKOBA YA KOCHA MKUU WA BENFICA

MOURINHO ATAJWA KUCHUKUA MIKOBA YA KOCHA MKUU WA BENFICA

55
0
mourinho

Jina la kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho linatajwa huenda likarejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati huu ambapo mazungumzo yanaendelea ili akinoe kikosi cha Benfica.

Benfica ilimtimua kocha wao siku ya Jumanne usiku kufuatia kipigo cha 3-2 walichokipata kutoka kwa klabu ya Qarabag ya Azerbaijani.

Kwenye mchezo huo Benfica ilitangulia kwa mabao 2-0 lakini iliruhusu wageni wao kupambana na kushinda mchezo huo.

Bruno Lage katika mwaka wake mmoja kama kocha wa Benfica, aliwaongoza kutwaa Kombe la Ligi ya Ureno na kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita.

Rais wa Benfica, Rui Costa amewaambia waandishi wa habari mapema leo kwamba ilikuwa muhimu kubadilisha kocha.

“Leo tumefikia makubaliano na Bruno Lage kujiuzulu kama mkufunzi wa Benfica … tunaamini ni wakati wa mabadiliko,” Rui Costa alisema.

“Kuhusu kocha ajaye, tunatarajia kuwa na mpya kwenye benchi Vila das Aves Jumamosi ijayo.

“Kocha wa Benfica lazima awe mshindi” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here