Home KITAIFA MAGORI AAHIDI KUIRUDISHA HESHIMA YA SIMBA

MAGORI AAHIDI KUIRUDISHA HESHIMA YA SIMBA

196
0
Magori

JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crecentius Magori, amesema yeye na wenzake wanakwenda kurudisha heshima ya klabu hiyo nchini na kuendelea kuwa ya kutisha na kuogopwa katika soka la Afrika.

“Simba ni klabu kubwa sana, ni klabu ambayo haina mfano Tanzania na Afrika Mashariki na Kati. Mimi na mwenzangu hapa mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, huyu bwana ni rafiki yangu sana, watu wanasema maneno mengi, achana na meno, achana na mambo yote, tunakwenda kufanya kazi kubwa na ya maana kwa ajili ya Simba.

“Kama kweli wewe ni Simba, tunashinda wote, tukikwama ni wote, hakuna kusema fulani amekwama. Nawaomba wanachama kuanzia sasa tuwe kitu kimoja, tupambane. Na yule ambaye hataki tuwe kitu kimoja kuisapoti Simba, tutammulika, ataonekana, atabaki wazi na atakimbia mwenyewe.”

Kwa hiyo ndugu zangu mikakati ni mingi, mapambano ni makubwa, lakini kwa kazi kubwa tutakayofanya, kwa kudra za Mwenyezi Mungu tutafanikiwa kwa pamoja kuivusha Simba yetu, kurudisha heshima yake kwenye soka la Tanzania na kuendelea kutisha Afrika nzima,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here