Home KIMATAIFA KINDA WA AJAX AVITOA UDENDA VILABU VIKUBWA DUNIANI

KINDA WA AJAX AVITOA UDENDA VILABU VIKUBWA DUNIANI

271
0
Ajax

Kinda wa Klabu ya Ajax, Aaron Bouwman anaripotiwa kuvivutia vilabu vikubwa duniani.

Kwa mujibu wa taarifa, kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 anafuatiliwa na Chelsea, Manchester United, Barcelona, ​​Liverpool na Manchester City.

Beki huyo wa kati alijiunga na Ajax mwaka 2018 na akacheza kwa mara ya kwanza Jong Ajax (timu ya pili ya Ajax) kwenye msimu wa 2023-24.

Baada ya kuwachezea mechi 15, kijana huyo ambaye ana baba Mholanzi na mama Mjamaika, amefuzu kwenye kikosi cha kwanza cha Ajax.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here