JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA
Kocha Mkuu wa klabu ya Simba Fadlu Davids amesema msimu huu ni wa kushinda makombe baada ya msimu uliopita kutengeneza kikosi chake kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya maandalizi ya tamasha la Simba Day siku ya kesho ambapo watacheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Gormahia Fadlu ameonekana kufurahishwa na usajili mkubwa walioufanya.
“Simba SC msimu uliopita tulitengeneza Foundation ila msimu huu ni wa kushinda makombe dirisha la usajili limeshafungwa, nawaamini sana wachezaji wangu wote na nimefurahishwa na kikosi changu. Kama kocha nitafocus na kikosi hiki kutengeneza timu yenye ushindani msimu huu.”- Fadlu Davids.