Home KITAIFA ALI KAMWE: SIMBA YA SAFARI HII NI MBOVU SANA

ALI KAMWE: SIMBA YA SAFARI HII NI MBOVU SANA

89
0

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa Simba SC ya msimu huu wa 2025/26  ni mbovu kuliko ile ya msimu uliopita wa 2024/25.

Yanga SC kwa sasa mkononi wana taji la Ngao ya Jamii walitwaa kwa kushinda mbele ya Simba SC mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 16 2025 ikiwa ni mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26..

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 1-0 Simba SC, bao la ushindi likifungwa na Pacome dakika ya 53 akiwa ndani ya 18 alipomtungua Moussa Camara kipa namba moja wa Simba SC.

Kamwe amesema: “Simba ya msimu huu ni mbovu zaidi kuliko ya msimu uliopita, ni mbovu kwa sababu wachezaji wapya hawana ubora wa kushindana naona wanapambana kutafuta matokeo uwanjani.

“Kwa hali ilivyo ninaona kabisa ndoto yangu ya kufikisha furaha ya kumfunga Simba SC mara kumi mfululizo nazidi kuiona na kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara nyingine tena,”alisema Kamwe.

Kikosi cha Yanga SC kwa sasa kipo nchini Angola ambapo kipo hapo kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya awali.

Yanga Ijumaa hii ya Septemba 19 watakuwa Uwanja wa Estadio 11 de Novembro wakicheza na Wiliete Sports Clube mechi ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa kuanzia saa 12:00 jioni ambapo Watanzania na dunia itashuhudia burudani hiyo  mubashara kupitia AzamSports1HD.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here