JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA
MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe ameahidi kuishitua Dunia Keshokutwa katika kilele cha Wiki ya Mwananchi itakayofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz ambaye ni mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi aliyekiongoza kikosi hicho kutwaa taji la ubingwa msimu wa 2024/25.
Ni Wiki ya Mwananchi ambayo inasubiriwa kwa shauku kubwa Septemba 12 2025 na Yanga SC inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Bandari ikiwa ni mwanzo wa msimu wa 2025/26.
Kamwe amesema: “Siku ya Wananchi hamjawahi kuniona kwenye kipaza wala eneo lolote nikifanya vurugu zangu ila mwaka huu nimo.
“Mimi ni kisima cha ubunifu na wote mnanijua. Nikishaingia hakuna binadamu yeyote atakayejadili entrance ya mtu mwingine zaidi yangu, nitaishtua Dunia,” alisema Kamwe.