Home KIMATAIFA Tatizo la Man U lipo kwa klabu sio wachezaji – Ruud Gullit

Tatizo la Man U lipo kwa klabu sio wachezaji – Ruud Gullit

145
0
man u

Gwiji wa soka wa Uholanzi, Ruud Gullit amesema tatizo la Manchester United lipo kwenye klabu na si kuhusu wachezaji.

Kulingana na gwiji huyo wa soka, tatizo la Manchester United ni Manchester United na si kwa wachezaji.

Alisema jinsi klabu imekuwa ikiendeshwa tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson, ndio tatizo lenyewe.

Kwa mujibu wa Gullit wachezaji walioihama klabu hiyo na kujiunga na vilabu vingine ndani ya kipindi hiki, wameenda kufanya vyema katika timu zao mpya, akiwatolea mfano Scott McTominay, [Napoli], Marcus Rashford, [Aston Villa, Barcelona] na Antony, [Real Betis].

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here