Home KITAIFA Siku ya kihistoria kwa Taifa la Tanzania ufunguzi wa michuano ya CHAN.

Siku ya kihistoria kwa Taifa la Tanzania ufunguzi wa michuano ya CHAN.

137
0

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars itashuka leo dimbani majira ya saa 2 usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Timu ya Taifa ya Burkina Faso kwenye mchezo wa kwanza wa kundi B katika ufunguzi wa mashindano ya CHAN 2024.

CHAN ni Mashindano yanayohusisha wachezaji wa ligi za ndani ambayo kwa mara ya kwanza yanafanyika Afrika Mashariki kwa ushirikiano wa Nchi tatu ambazo ni Tanzania Kenya na Uganda huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa mchezo wa ufunguzi.

Tanzania inakutana na Burkina Faso ambayo haijawahi kupata ushindi dhidi ya Taifa Stars wakiwa nyumbani katika michezo mitatu ya mwisho waliyokutana nayo hivi karibuni tangu mwaka 2006.

Taifa Stars imeshinda mara mbili 2 dhidi ya Burkina Faso mchezo mmoja wakishinda wakiwa nyumbani na mmoja ugenini huku Burkina Faso wakipata ushindi mara moja wakiwa ugenini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here