Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta anatarajia kucheza mechi yake ya kwanza kwenye Ligi Kuu Ufaransa wakati klabu yake ya Le Havre itapokutana na AS Monaco.
Samatta siku ya leo endapo akipata nafasi ya kuitumikia timu yake atakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kukiwasha katika ligi hiyo akicheza dhidi ya nyota wa zamani wa Man U na Barcelona Paul Pogba na Ansu Fati wanaoitumikia As Monaco kwa sasa.