Home KITAIFA HUYU HAPA KUULIZWA IKIWA SIMBA SC ITABUMA MSIMU MPYA

HUYU HAPA KUULIZWA IKIWA SIMBA SC ITABUMA MSIMU MPYA

541
0

KUELEKEA msimu mpya wa 2025/26 ni Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC ameachiwa msala kwenye suala la usajili baada ya kupewa jukumu hilo kuhakikisha kwamba kila kitu anasimamia mwenyewe.

Simba SC imeweka kambi Misri kwa maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku wakifanya usajili wa wachezaji wapya ikiwa ni Jonathan Sowah aliyekuwa Singida Black Stars, Morice Abraham, Anthony Mligo na kuna wengine wapo kwenye majaribio.

Kitendo cha mabosi wa Simba SC kubainisha kuwa ambaye anasimamia usajili kwa asilimia 100 ni sawa na kumuachia msala kocha huyo jambo lolote likitokea kwa wachezaji kufeli mzigo ataangushiwa yeye.

Advertisement

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa suala la usajili kwa Simba SC lipo mikononi mwa benchi la ufundi.

“Benchi la ufundi linasimamia suala la usajili kwa kila hatua hivyo kwa wakati huu tumeamua iwe hivyo na kila usajili unaofanyika unafuatiliwa kwa umakini na benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here