Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba amethibitisha kuwa mchezaji wao mpya ameanza kwenye kikosi cha timu yake ya Taifa katika mashindano ya CHAN na ndiye atakayekuwa Nahodha wa Taifa lake.
“Mchezaji wetu mpya anaanza kwenye mechi ya Taifa lake na tena ndio nahodha…. Automatic hii timu yetu ya pii kushangilia kwenye CHAN”Ameandika Ahmed Ally.
Ikumbukwe klabu ya Simba inatajwa kumalizana na mchezaji wa Mamelodi Sundowns Neo Maema ambaye ndiye Nahodha wa Afrika Kusini kwenye mchezo wa leo dhidi ya Algeria.