Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿 Dkt. Samia Suluhu Hassan atatoa kiasi cha shilingi Bilioni 1 Endapo Tanzania ‘Taifa Stars’ itabeba ubingwa wa mashindano ya CHAN 2024 yatakayoanza kutimua vumbi Agosti 2 mwaka huu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amethibitisha hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya michuano hiyo kwenye dimba la Benjamini Mkapa siku ya leo.
“Naomba niutangazie umma wa Tanzania kuwa katika kuchagiza hamasa kwa Timu yetu ya Taifa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi ya donge nono la fedha Shilingi Bilioni siyo Milioni Bilioni 1 kwa vijana wetu wa Taifa Stars iwapo watafanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano haya ya CHAN” Amesema Waziri Kabudi.