KITAIFA

USIKIE MKWARA WA YANGA KUHUSU DIRISHA HILI LA USAJILI?

UONGOZI wa Yanga SC umeweka wazi kwamba kazi inaanza kwenye usajili kwa kuwa kuna wachezaji wengine wa maana watatambulishwa hivi karibuni.

Mpango mkubwa wa Yanga SC ulikuwa ni kufungua ukurasa Julai 22 kutambulisha wachezaji wapya ila ngoma ilibadilishwa hewani baada ya kufungua ukurasa rasmi Julai 18.

Ni Moussa Conte alitambulishwa na Yanga SC ikiwa ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa Yanga SC ambao ni mabingwa wa ligi kuelekea msimu wa 2025/26.

Ali Kamwe ameweka wazi kuwa huo ni mwanzo watatambulisha wachezaji wengine wakubwa na wenye uwezo ili kuendelea pale ambapo waliishia msimu wa 2024/25.

“Huu ni mwanzo, niliona kwamba wanasema wamekamilisha usajili wa mchezaji fulani, tunasubiri tuone itakuaje huko kwao. Ambacho tumekifanya ni mwanzo tu kazi bado inaendelea.”

Mchezaji huyo Conte alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba SC walipishana naye inatajwa kwenye upande wa dau akasaini Yanga SC.

Leave a Comment