Yanga SC imekamilisha usajili wa kiungo wa CS Sfaxien ya Tunisia Balla Conte akiwa ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa na mabingwa hao watetezi.
Conte rasmi ni njano na kijani baada ya kutambulishwa na Yanga SC, Julai 18 2025 tayari kwa maandalizi ya msimu wa 2025/26.
Ikumbukwe kwamba nyota huyo alikuwa anatajwa kuwa katika rada za watani wa jadi wa Yanga SC ambao ni Simba SC nao walikuwa kwenye hesabu za kuwania saini yake.
Hivyo vita ya watani hawa wa jadi imegota mwisho na Yanga SC akiwa mshindi kwenye vita ya kwanza ya usajili kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Yanga SC walianza na ujumbe kuwa ni kishindo cha bilioni 87 ambacho kinakuja kwa mabingwa hao wa ligi wakiwa na mataji 31 kibindoni.