Nzengeli Afanya Mazoezi na Yanga Princess

nzengeli

Wakati huu programu za mazoezi za timu za Ligi kuu wanaume zikiwa zimesimama na wachezaji wengi wakiwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa kwenye michuano ya AFCON huku wengine wakiwa mapumziko, mchezaji kiraka wa Yanga SC Max Ngengeli ameonekana akifanya mazoezi va timu ya wanawake ya Yanga.

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii Yanga Princess jana walichapisha picha za Max akifanya mazoezi na timu hiyo inayojiandaa na mechi ya Ligi kuu wanawake itakazoendelea kesho tarehe 22 dhidi ya Geita Gold Queens.