JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA
Mabingwa wa zamani wa dunia katika masumbwi, Mike Tyson na Floyd Mayweather, wanatarajiwa kukutana ulingoni kwa pambano la maonyesho mwaka 2026.
Kampuni ya yenye kujihusisha na mchezo wa masumbwi, CSI Sports, imetangaza pambano hilo kati ya Tyson, ambaye atatimiza miaka 60 mwaka ujao, na Mayweather mwenye umri wa miaka 48.
Hata hivyo mpaka sasa bado hakuna taarifa kuhusu mahali ambapo pambano hilo litafanyika wala tarehe rasmi ya tukio hilo.
Tyson, bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani, alishindwa kwa pointi dhidi ya Jake Paul katika pambano la raundi 8 lililofanyika Novemba 2024. Floyd Mayweather alitwaa mataji ya dunia katika aina tano ya viwango vya uzito tofauti, na hakuwahi kushindwa katika mapambano yake 50.