Kiungo nyota wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane, amekubali rasmi kurithi mikoba ya Didier Deschamps kama Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa, Zidane anatarajiwa kuchukua jukumu hilo mara baada ya michuano hiyo itakayofanyika katika mataifa ya Marekani, Mexico na Canada.
Kocha wa sasa, Deschamps, amekuwa akiinoa Ufaransa tangu mwaka 2012, lakini tayari ameshaweka wazi kuwa ataachia ngazi baada ya Kombe la Dunia lijalo. Hatua hiyo itahitimisha safari yake ya miaka 14 yenye mafanikio makubwa akiwa na kikosi hicho.
Katika kipindi chake, Deschamps aliiongoza Ufaransa kufika fainali ya UEFA Euro 2016 pamoja na fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar.
Uteuzi wa Zidane unatajwa kuwa mwanzo mpya kwa timu hiyo, huku mashabiki wengi wakitarajia kuona mafanikio zaidi chini ya nahodha huyo wa zamani aliyewahi kuipa Ufaransa heshima kubwa akiwa mchezaji.
