Mshambuliaji wa klabu ya Simba Elie Mpanzu amefunguka sababu iliyomfanya aongeze mkataba wa kuitumikia klabu yake ya sasa akiweka wazi ni kutokana na upendo alioupata kwa wanasimba kipindi anapitia nyakati ngumu.
“Nikiwa na machozi machoni mwangu ninawaandikia, wapenzi mashabiki wa Simba. Ninyi ndio wafuasi bora zaidi ambao nimewahi kukutana nao. Nataka kuwashukuru kutoka moyoni mwangu kwa msaada wenu usioyumba, licha ya nyakati ngumu ambazo nimepitia. Mmekuwa mkiniamini kila wakati,
“N kutokana na maombi yenu, simu, ujumbe, kutia moyo kwenu, na ushauri wenu kwamba ninaanza kurudi kwenye mstari. Ndiyo maana nimeamua kutowasaliti na kuendelea na klabu. Ninawapenda nyote sana na ninawaahidi mambo mema katika siku zijazo”. Ameandika Elie Mpanzu.
