Home KITAIFA MBEYA DAY NI LEO KUNOGESHWA NA MECHI KALI DHIDI YA AZAM FC

MBEYA DAY NI LEO KUNOGESHWA NA MECHI KALI DHIDI YA AZAM FC

84
0

JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA

PAZIA la Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora linakaribia kufunguliwa ikiwa ni siku zinahesabiki kwa kuwa Septemba 17 kazi inatarajiwa kuanza.

Leo kuna tamasha kubwa nyanda za juu Kusini, ambapo Mbeya City iliyorejea kwa mara nyingine ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika watakuwa na jambo lao.

Mbey City, The Purple Nation,  Uwanja wa Sokoine, Mbeya watafanya utambulisho wa kikosi chao cha msimu wa 2025/2026 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Miongoni mwa wachezaji waliopo Mbeya City ni kipa wa zamani wa Simba SC na Yanga SC, Beno Kakolanya ambaye yupo hapo kwa mara nyingine tena katika kutimiza majukumu yake.

Kutakuwa na mchezo mkali wa kirafiki kati ya wenyeji Mbeya City dhidi ya matajiri wa Dar, Azam FC ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kocha Msaidizi wa Mbeya City Mussa Rashid ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na watatoa burudani nzuri kwa mashabiki watakaojitokeza.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo na wapinzani wao Mbeya City wamefanya makosa kuichagua Azam FC kwa kuwa ina hasira kutafuta matokeo hata kama imealikwa.

Mgeni rasmi kwenye tamasha hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa atashuhudia burudani zote kwenye tukio hili kubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here