Home KITAIFA SAFU MPYA YA UONGOZI SIMBA SC IPO HIVI

SAFU MPYA YA UONGOZI SIMBA SC IPO HIVI

183
0
Simba

JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA

MO Dewji amemteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba SC hivyo mipango yote itakuwa inaendelea chini ya safu mpya ya uongozi.

Mo amebainisha kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na  kuhudumu kwa muda mrefu na majukumu yake akiwa mbali ameone ni muhimu Klabu ya Simba SC ipate kiongozi wa bodi ambaye yupo karibu na mwenye muda wa kutosha ambaye anaweza kushiriki kwa ukaribu kabisa shughuli za kila siku.

Kwa mujibu wa taarifa ya MO yeye atasalia kuwa muwekezaji na Rais wa Simba SC huku akiteua wajumbe wengine wa bodi.

Ni Swedi Mkwabi ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Simba SC, Azim Dewji, Hussein Kitta, Rashidi Shangazi, Zully Chandoo, Barbara Gonzalez aliyewahi kuwa CEO wa Simba SC na George Ruhango.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here