Home KIMATAIFA Paul Pogba rasmi kukiwasha ligi ya Mabingwa Ulaya.

Paul Pogba rasmi kukiwasha ligi ya Mabingwa Ulaya.

132
0
Paul Pogba participates in the pre-season 2025-2026 match between Monaco and Inter in Monaco, Monaco, on August 8, 2025. (Photo by Loris Roselli/NurPhoto) (Photo by Loris Roselli / NurPhoto via AFP)

JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA

Klabu ya AS Monaco imemjumuisha mchezaji Paul Pogba katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2025/26.

Pogba ambaye alijunga na Monaco kama mchezaji huru mwishoni mwa mwezi Juni baada ya kumaliza kifungo chake cha miaezi 18 alichohukumiwa kwa kosa la kutumia madawa yaliyozuiliwa michezoni anatarajia kurejea uwanjani rasmi mwezi octoba akiwa na timu yake mpya.

Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United ataikosa michezo miwili ya klabu hiyo kwenye mashindano hayo Septemba 18 dhidi ya Club Brugge na Octoba 1 dhidi ya Manchester City.

Endaapo atapata nafasi ya kucheza katika michano hiyo itakuwa mara yake ya kwanza kushiriki tena katika michuano hiyo tangu Machi 2022 alipokuwa akiichezea Manchester United.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here