Home KITAIFA RAIS WA CAF AMPONGEZA RAIS WA TFF KWA KUREJEA TENA MADARAKANI

RAIS WA CAF AMPONGEZA RAIS WA TFF KWA KUREJEA TENA MADARAKANI

17
0

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dk. Patrice Motsepe ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kuchaguliwa tena katika nafasi hiyo.

“Kuchaguliwa kwako tena ni ishara ya imani ya Wanachama wako kwa uongozi wako bora, najivunia sana bidii yako na kujitolea kwa maendeleo na ukuaji wa soka Tanzania,” alisema Dk. Motsepe.

Vilevile ameipongeza Kamati ya Utendaji iliyochaguliwa, na amesema CAF itaendelea kusaidia kukuza mpira wa miguu Tanzania na Kanda ya CECAFA (Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati).

Advertisement

Uchaguzi wa kupata Kamati mpya ya Utendaji ya TFF ulifanyika Agosti 16 mwaka huu jijini Tanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here