Ruka hadi maudhui
SOKALEO

ROONEY AMTABIRIA MABAYA ARTETA, AMSHAURI APIGE KAZI

Chikao
ROONEY AMTABIRIA MABAYA ARTETA, AMSHAURI APIGE KAZI

GWIJI wa Ligi Kuu England, Wayne Rooney, ameonya kuwa Mikel Arteta anaweza kufukuzwa kazi endapo atashindwa kuipa Arsenal taji la Ligi Kuu msimu huu 😳🏆

Arsenal kwa sasa inaongoza ligi kwa pointi sita mbele ya Manchester City, na imekuwa vinara wa kubashiriwa kushinda taji lao la kwanza tangu mwaka 2004. Kwa mujibu wa Rooney, nafasi hiyo nzuri inaondoa kabisa visingizio kwa Arteta.

Akizungumza kwenye kipindi cha The Wayne Rooney Show, amesema: “Arsenal wamemuunga mkono Arteta kwa kiwango kikubwa na wamempa kikosi bora sana. Kama hawatashinda mwaka huu, kutakuwa na presha kubwa kwake, bila shaka.”

Rooney pia anaamini ushindi wa kusisimua wa Man City dhidi ya Liverpool Anfield unaweza kuwa umeathiri kisaikolojia kikosi cha Arteta. City ilirejea kutoka nyuma na kushinda 2-1, hali iliyopunguza pengo kutoka pointi tisa hadi sita.

Je, Arteta atakamilisha kazi au presha itamlemea?

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Vigogo wa Ulaya Kukipiga Leo Kwenye UEFA

Dani Carvajal aondoka Madrid baada ya miaka 23

MICHAEL OWEN: Ni mapema mno kumfukuza Carrick Manchester United

Kunyoa kumenipa faragha mtaani, watu hawanitambui – Haaland