Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, amezungumzia maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa kesho Jumatano, Februari 11 kwenye uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam saa 1:00 usiku kwa muda wa Tanzania.
Barker amesema maandalizi ya kikosi chake yamekwenda vizuri hadi sasa, na amesisitiza umuhimu wa kucheza mchezo huo kwa kiwango cha juu ili kupata ushindi unaotakiwa.
“Tunahitaji kucheza mechi hii vizuri ikiwa ni pamoja na kutawala mchezo na kupata ushindi kama ambavyo malengo yetu yalivyo,” amesema kocha huyo raia wa Afrika Kusini.
Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa na hamu kubwa ya kuendeleza mfululizo wa matokeo mazuri na kuimarisha nafasi yake katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.