Home KITAIFA KOCHA FADLU AFUNGUKA MIPANGO YAKE KWENYE NGAO YA JAMII

KOCHA FADLU AFUNGUKA MIPANGO YAKE KWENYE NGAO YA JAMII

376
0
fadlu

Kocha wa Simba SC ameweka wazi msimamo na mikakati ya kikosi chake kuelekea mchezo muhimu wa ngao ya jamii dhidi ya Young Africans (Yanga).

Akizungumza baada ya mapumziko mafupi, kocha huyo amesema kikosi chake kimeanza maandalizi mapya kwa mchezo huo wa heshima kabla ya kuelekeza nguvu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tumepumzika jana na kisha leo tunaanza maandalizi ya mechi ya Yanga. Huo ni mtihani mkubwa, ni fainali, ni mechi ya heshima. Baada ya hapo tutaelekeza nguvu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Tutafanya uchambuzi, mikutano binafsi na ya pamoja, ili kuweka mambo sawa,” alisema kocha.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa mashabiki kuendelea kutoa sapoti kubwa, akibainisha matarajio ya timu kupata kibali cha kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi za nyumbani ili mashabiki wengi waweze kushuhudia michezo yao.

“Naamini Ligi Kuu itaturuhusu kucheza mechi zetu za nyumbani kwa Mkapa kwa sababu mashabiki wengi zaidi wataweza kutuona. Tunahitaji msaada wao zaidi wiki ijayo, nusu ya uwanja uwe mwekundu. Hizo ndiyo mechi kubwa zinazohitaji umoja wa mashabiki na wachezaji,” aliongeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here