“Nimeona andiko la kaka yangu Jemedari Said kuzihusu Simba SC na Azam FC kutokutoa matokeo yao ya mechi zao za kirafiki walizocheza.
Azam FC walifungwa 2-1 na JKT Tanzania pale Arusha. Simba SC wakafungwa 4-3 na Enpipp pale Misri. Kwangu ni tofauti kidogo.
Nasimama na Azam FC na Simba SC waliochagua kukaa kimya na taarifa za matokeo ya mechi zao. Kuna kitu kinaitwa mechi za Indoor. Hizi ni mechi ambazo hazina mashabiki. Hazitakiwi kutoka nje ndio maana zikaitwa Indoor.
Makocha wanapenda kuzitumia mechi hizi kwa ajili ya kutazama mbinu zao zinafanyaje kazi. Timu zetu huwa zinacheza sana mechi zenye sura hii.
Simba ambao walifungwa juzi, walicheza mechi nyingine na walishinda, lakini hawajapost matokeo ya mechi katika ukurasa wao na hata mtu mmoja aliyehoji.
Hata waliotoa taarifa ya mechi ile ambayo Simba SC walishinda walipata shida kupata matokeo. Lakini hi haikuonekana kama ni shida.
Kilionekana kitu cha kawaida tu. Kama Simba wangetoa matokeo ya mechi ile waliyoshinda, kisha hawajapost matokeo ya mechi ya juzi, ingeleta shida kwa wapenzi wao na moja kwa moja tungesema wanachagua taarifa za kuzitoa.
Lakini walivyoshinda hawajatoa matokeo. Kwanini tuhoji walivyofungwa? Mimi naamini hizi ni mechi ambazo zipo sana na zinachezwa sana pale Avic Town. Bunju Arena. Chamazi. KMC Complex zinachezwa sana, tena kila siku au nyingine asubuhi na nyingine jioni. Ni mechi za kawaida mno. Ni kawaida sana.
Binafsi nimewahi kushuhudia mechi zenye sura hii nyingi tu zilizokosa idadi. Tena nimetazama mechi za Simba SC na Yanga SC matokeo yake yanabaki ndani pale pale” Ameenda Mkunga