Home KITAIFA USAJILI WA KWANZA SIMBA HUU HAPA, MSHAMBULIAJI WA MABAO KUTAMBULISHWA

USAJILI WA KWANZA SIMBA HUU HAPA, MSHAMBULIAJI WA MABAO KUTAMBULISHWA

434
0

MSIMBAZI kumeanza kumechangamka kupitia usajili baada ya dirisha la usajili kufunguliwa huku wakiwa hajatangaza mchezaji hata mmoja mpya ambaye ameshasaini kandarasi Simba SC.

Mabosi wa Singida Black Stars, wameeleza kuwa Jonathan Sowah ambaye ni mshambuliaji wao wameingia makubaliano ya kumuuza ndani ya Simba SC kwa makubaliano maalumu.

Hivyo Sowah anakuwa nyota wa kwanza usajili wake kuwekwa wazi baada ya timu ya Simba SC kuwa kwenye sarakasi nyingi kutokana na wachezaji ambao walikuwa wanatajwa kuwa kwenye hesabu za Kocha Mkuu, Fadlu Davids kutambulishwa kwa timu pinzani ambayo ni Yanga SC.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wanatajwa kuwa kwenye hesabu za Simba SC wakatambulishwa Yanga SC ni kiungo Ballac Conte ambaye kasaini dili la miaka mitatu Jangwani.

Imeelezwa Sowah anakuja kuchukua nafasi ya straika Lionel Ateba ambaye anatarajiwa kutimkia uarabuni. Imethibitishwa kuwa Simba walikamilisha dili la Sowah usiku wa kuamkia Jumatano Julai 16 2025.

Ikumbukwe kwamba kwa msimu wa 2024/25 Sowah kwenye ligi ikiwa ni ingizo jipya katika dirisha dogo alifunga jumla ya mabao 13 akiwa na Singida Black Stars ambayo ilicheza fainali ya CRDB Federation Cup dhidi ya Yanga SC ikapishana na taji hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here