Home KITAIFA FEISAL KUONDOLEWA KWENYE MIPANGO YA SIMBA?

FEISAL KUONDOLEWA KWENYE MIPANGO YA SIMBA?

1169
0

WAKATI jina la kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum likitajwa kuwa miongoni mwa wale ambao wamefuatwa kwenye sanduku la usajili la Simba SC katika kina cha Bahari ya Hindi inaelezwa kuwa jina hilo halipo.

Taarifa zinaeleza kuwa jina la Fei limekutana na ugumu mzito kuwa ndani ya Simba SC hivyo jitihada zinaendelea kufanyika mpango ukiwa sawa utaratibu utafuatwa ili jina lake liongezwe katika orodha.

Ikumbukwe kwamba Fei ana mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC amekuwa akitajwa kuwa katika rada za Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids.

Simba SC leo Julai 29 2025 ina jambo lake katika Hotel ya Johari Rotana ambapo taarifa zinaeleza kuwa kuna mdhamini mpya ambaye atatambulishwa.

Kampuni moja kubwa inatarajiwa kutambulishwa kuwa mdhamini mkuu wa Simba SC kwa msimu wa 2025/26 huku wakitajwa kusitisha mkataba na moja ya kampuni kubwa iliyokuwa inawadhamini Simba SC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here