KITAIFA

BEKI YANGA SC MKATABA WAKE UMEKWISHA, ATAJA ATAKAPOSAINI

yanga

BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga SC Dickson Job huenda akaongeza kandarasi nyingine ndani ya kikosi hicho. Nyota huyo mkataba wake msimu wa 2024/25 unagota mwisho.

Kwa sasa bado hajaongeza mkataba mwingine na inaelezwa kuwa mazungumzo yameanza kwa pande zote mbili. Juni 29 2025 ulikuwa ni mchezo wa mwisho kwa msimu wa 2024/25 hivyo jambo lake litafanyiwa kazi haraka.

Uongozi wa Yanga SC uliweka kando mazungumzo na wachezaji wengi kutokana na mechi ngumu ambazo zilikuwa juu yao. Kariakoo Dabi Juni 25, Yanga SC 2-0 Simba SC na fainali ya CRDB Federation Cup Juni 29, Yanga SC 2-0 Singida Black Stars.

Mara baada ya Yanga SC kutwaa taji la CRDB Federation Cup, beki huyo aliweka wazi kuwa mkataba wake unaisha hivyo itafahamika wapi atakuwa.

“Kikubwa tusubiri kwa sababu ninakwenda kumaliza mkataba hayo mengine yakiwa sawa kila mtu atajua. Kila kitu kinawezekana kikubwa ni maelewano na mazungumzo mazuri,” alisema Job.

Leave a Comment