Home KIMATAIFA Chelsea kwenye mazungumzo na Man U ili kumnunua Alejandro Garnacho

Chelsea kwenye mazungumzo na Man U ili kumnunua Alejandro Garnacho

49
0

Manchester United na Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya kuuziana mchezaji Mu-Argentina Alejandro Garnacho.

United inamthaminisha Alejandro mwenye umri wa miaka 21 kwa Pauni milioni 50, ingawa Chelsea wanaamini wanaweza kujadiliana na kumpata kwa bei ya chini zaidi.

Garnacho ameambiwa atafute klabu mpya na mabosi wa United na aliondolewa katika ziara ya Marekani na kocha Ruben Amorim.

Advertisement

Amekuwa akifanya mazoezi nje ya kikosi cha kwanza tangu kikosi hicho kiliporejea Carrington siku ya Jumanne.

Winga huyo wa Argentina ameweka wazi kuwa anachopendelea ni kuhamia Stamford Bridge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here