Home KITAIFA TAIFA STARS KAMILI KUWAKABILI MAURITANIA KWA MKAPA AGOSTI 6 2025

TAIFA STARS KAMILI KUWAKABILI MAURITANIA KWA MKAPA AGOSTI 6 2025

75
0
taifa stars

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemedi Selemani, amesema kuwa ana imani kubwa na kikosi kuelekea mchezo unaofuata wa Agosti 6, 2025 dhidi ya Mauritania unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Kocha huyo amesisitiza kuwa lengo kuu ni kupata ushindi bila kujali idadi ya mabao kwenye mchezo wa leo unaotarjiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Suleiman amesema kuwa ushindi ndio jambo la msingi zaidi katika mashindano ndani ya uwanja jambo ambalo wanalitarajiwa baada ya dakika 90 za mchezo.

Advertisement

“Naamini sana katika kupata ushindi haijalishi tutafunga magoli mangapi cha msingi ni kupata ushindi. Wachezaji wapo tayari na morali ni kubwa kuelekea kwenye mchezo wetu muhimu na tunawaheshimu wapinzani wetu.”

Tanzania kwenye mchezo wa kwanza ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso, mabao yalifungwa na Sopu na Mohamed Hussen Zimbwe Jr.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here